VicobaStore: Mfumo huu ni mahususi kwa ajili ya hifadhi taarifa za fedha za vikundi vya kijamii kama vile vicoba, taasisi au mtu binafsi, unaweza hifadhi taarifa za mikopo, jamii, hisa, mapato na matumizi ya kikundi, pia wakopeshaji binafsi wanaweza tumia. Kwa kutumia mfumo huu kunakuwa na uwazi wa taarifa za kikundi kwani kila mwanachama anaweza kuona taarifa zote za fedha, Hivyo mhazini anakuwa amepunguziwa kazi ya kuandaa taarifa za fedha kila wakati.
Miamala
☛Kuweka fedha kwenye akiba, hisa na jamii kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake
☛Kutoa fedha kwenye akiba, hisa na jamii kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake
☛Mikopo (kukopesha, kurejesha na kufuta mkopo kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake)
☛Kuhifadhi mapato na matumizi ya kikundi
☛Kuhamisha fedha kutoka taslimu kwenda benk/kutoka benki kwenda taslimu
-Marejesho ya mkopo ni automatically, ila kuna option ya kulipa mannually
Ripoti
☛Mikopo yote ya kikundi na kuonesha salio la msingi, malimbikizo na riba ghafi
☛Orodha ya masalio ya akiba, hisa na jamii
☛Taarifa ya mapato na matumizi
☛Salio la fedha taslimu na kiasi kilichopo benki
☛Orodha ya michango yote kama rejesho,hisa,akiba na jamii kwa ajili ya kupost kila mwisho wa mwezi, hivyo mhasibu hana haja ya kuandaa orodha nyingine kwa ajili ya ku *post*
☛Riba ghafi(accrued interest) kwenye akiba zako ambayo inakuwa automatically calculated on daily basis, hii ndio inayotumika kwenye tathimini ya gawio.
☛Idadi ya wanachama wote
NB: Mwanchama ambaye si mhasibu atakuwa anauwezo wa kuona taarifa zake zote kama vile
☛Salio la akiba
☛Salio la hisa
☛Salio la jamii
☛Taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi
☛Idadi ya wanachama wote wa kikundi